Inuka Tena
Matatizo ya kihisia yanaweza kusababishwa na mambo kadhaa mfano kwenye familia, kazini, mahusiano na hata kwenye jamii inayotuzunguka.
Wengi wamekumbwa na matatizo ya kihisia na ndani ya mioyo yao kuna majeraha na hawajui hatima zao za kihisia na kiakili zitakwisha lini. Matokeo ya kihisia ni mlolongo uliopo kwenye akili na ufahamu wa mtu, namna akili na ufahamu ulivyochukua nafasi kwa muda mrefu ndipo matatizo ya kihisia huchukua nafasi.
Ushawahi kukutana na mtu anakwambia “nakupenda ila hisia na wewe sina?”, watu wenye mahusiano au waliowahi kupitia hali kama hiyo wanaweza kuungana na mimi katika hili, na kama hakuna hisia hakuna mapenzi.