Linda Thamani ya Jina Lako
Kitabu hiki cha Linda Thamani Ya Jina Lako ni kitabu kipya kitakachokuweza kujifunza mengi juu ya kulinda kile ambacho Mungu amekiweka katika maisha yako. Karibu ujipatie nakala yako.
Ni kitabu kizuri ambacho kimejikita katika kuwaelimisha watu juu ya umuhimu wa kulinda majina yao. Jina lako ni utambulisho wako. Yapo mambo ambayo huharibu jina la mtu na kuonekana hafai katika jamii. Lakini pia yapo mambo ambayo ukiyafanya huongeza thamani ya jina lako.
Zakayo kabla ya kukutana na Yesu Kristo alifahamika kama mla rushwa, tapeli, mtoza ushuru, mnyang'anyi na kila aina ya jina baya watu walimwita. Baada ya kukutana na Yesu akiwa amepanda juu ya mti, Zakayo alikubali kubadilika na kuwa mtu wa tofauti na maisha aliyoishi hapo mwanzo.Rejea Luka 19:1-10. Watu wakisikia jina lako nini hasa cha kwanza huwajia katika ufahamu wao? Au watu wanakuzungumziaje? Wewe ni nabii. Tena nabii wa mataifa, ndivyo Mungu anavyojua. Je, huo unabii aliokuumba nao Mungu bado unao? Ni muhimu sana kulinda thamani ya jina lako.
Ndani ya kitabu hiki utajifunza juu ya maono, dhambi kama ukuta wa hatima yako, kuwapenda watu wa nyumbani mwako, unyenyekevu umewapa kibali watu wengi, kujifunza kwa watu wengine, kutokurudi nyuma baada ya kumkiri Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wako na kuwasamehe watu waliokukosea.