Usiishie Njiani
Kuweka kituo mahali ambapo Mungu ameweka mkato sio uwamuzi sahihi. Kila mtu kwa wakati tofauti hukutana na magumu na changamoto nyingi zenye kukatisha tamaa katika safari yoyote ya mafanikio. Hofu, mashaka, kutokujiamini, kukosa Imani ni vitu ambavyo mbeba maono yoyote atakutana navyo katika safari yake ya kutimiza maono hayo.
Wewe sio wa kwanza kushindwa kwenye harakati za utafutaji. Hivyo usijichukie wala kujilaumu ama kutafuta wa kulaumu. Giza linapokuwa kubwa ujue basi asubuhi imekaribia, hebu zidi kupiga hatua na usikubali kuishia hapo ulipo. Jambo la kutisha duniani sio kubadili uelekeo au mbinu za kiutafutaji bali ni kupoteza shauku. Kuanguka kwenye maji haimanishi umezama bali kukubali kukaa ndani ya maji basi umeamua kuzama.
Lakini avumiliaye mpaka mwisho ndiye atakayeokoka (Mt 24:13). Kuvumilia mpaka mwisho ndicho kitu Muumbaji wako anataka, amekuamini na amekutuma kutimiza hiyo ndoto uliyonayo. Mazingira yatakuvunja moyo, mchakato utakuumiza lakini usikubali kuishia njiani. Taji la ushindi lipo mwishoni, usikubali kuitwa mshiriki kwa kuishia njiani, bali hakikisha unafika mwishoni unaitwa mshindi na kuvalishwa taji.
Ndani ya kitabu hiki “USIISHIE NJIANI” utapata maarifa yatakayoinua shauku yako, maarifa yatakayorejesha tumaini lako na kukuwezesha kusonga mbele kutimiza ndoto zako.