Siri za Uhakika wa Ushindi katika Vita ya Kiroho na Jinsi inavyowatesa wengi
Vita ya kiroho ni mapambano katika ulimwengu wa roho kati ya nguvu za NURU dhidi ya nguvu za GIZA na vita hii ni halisi kabisa katika ulimwengu huu wa watu wenye miili lakini kwa kukosa ufahamu na uelewa wa vita hii,ili limekuwa tatizo ambalo limeendelea kuwatesa wakristo wengi pamoja na kanisa kwa ujumla wake.Shetani na washirika wametumia nafasi hii kuwashambulia watu wengi kwa njia mbali mbali za wazi na nyingine ni za kujificha sana,pamoja na mashambulizi hayo dhidi ya kanisa na wakristo lakini Mungu amewapa watu wake mamlaka na uwezo mkubwa wa silaha nyingi zaidi ya maelfu kwa ajili ya kujilinda na kumshambulia shetani.Lakini tatizo kubwa lililopo kwa kanisa na wakristo wengi ni ufahamu wa vita yenyewe ya kiroho,utambuzi wa silaha na namna ya kuzitumia kwa ufanisi katika kumshinda shetani.
Nimeandika kitabu hiki ili kuwasaidia na kuwajengea uwezo wakristo juu ya ufahamu na uelewa wa ukweli wa vita ya kiroho ili waweze kujitegemea katika mapambano dhidi ya shetani na washirika wake.Naimani kwa njia ya kitabu hiki kanisa pamoja mkristo wataweza kujua njia mbali mbali ya kuziona silaha maelfu za kivita zilizopo katika Biblia,jinsi ya kumtambua adui,uelewa mpana juu ya vita ya kiroho na nguvu za giza,falsafa mbali mbali katika vita ya kiroho,utambuzi wa silaha mbali mbali katika vita ya kiroho,jinsi ya kutumia silaha mchanganyiko katika vita ya kiroho,kutumia silaha ya malaika katika maombi na uhakika wa kushinda katika vita ya kiroho.