Faida za kutumika katika maono ya mtu mwingine
Katika siku za hivi karibuni kumeibuka mtazamo sio mzuri sana kuhusu kuajiriwa. Watu wamefundishwa kufikiri kwamba kuajiriwa ni kitu kibaya. Kimsingi watu wanafikiri kuajiriwan ni kumtajirisha aliekuajiri. Lakini kwa kweli hakuna kitu kizuri kama kuanzia kwenye kazi/maono ya mtu mwingine. Makosa mengi ambayo tunayafanya kwenye maono yetu mara nyingi inakuwa ni gharama ya kukosa uzoefu ambao kwa usalama Zaidi tungeupata kwenye kazi za watu wengine. Na kuwa huwezi kuwaambia watu wakufuate kama wewe hauna mtu unaemfuata au hujawahi kumfuata. Ndio maana nimeandika hiki kitabu hiki. Si ili kukuonesha faida za kutumika katika maono ya mtu mwingine bali namna nzuri ya kutumika katika maono ya mtu mwingine.