Kitabu
hiki ni mgodi uliosheheni madini kwa ajili ya mtu anayependa kuwa na matokeo
maishani. Majira mapya ni majira ya baraka, ni majira ya kicheko, ni majira ya
kukumbukwa na majira ya kutembea katika kusudi la kuumbwa kwako. Kitabu hiki
kinakupa tafsiri pana ya majira na tabia za mtu anayeweza kutembea katika
majira mapya. Kinachambua kwa kina kuhusu dalili za mtu aliye tayari kuingia
katika majira mapya na kukupa namna ya kuyafungulia majira hayo. Ili ufaidike
na majira mapya, ni sharti ujue jinsi gani uishi ndani yake, ukilijua hilo,
daima utakuwa ni mtu wa kupiga hatua kuelekea mbele na kamwe si nyuma.