Siri Iliyojificha Juu ya Uzinzi na Uasherati
Kitabu hiki kitakusaidia kuelewa mambo mazito ambayo yamejificha katika tendo hili, Mbinu anazotumia shetani kuwaingiza vijana ili kuharibu ubaadae wao, na pia utajifunza njia sahihi za kuchomoka katika hivyo vifungo na nini ufanye ili uweze kuchomoka huko.
Tumehubiriwa sana kuhusu dhambi ya uzinzi na uasherati. Wakristo hupata ufahamu mdogo na wa juu juu na kujiona wako salama kabisa Ndio maana kuna msemo " Garbage in garbage out". Injili ikihubiriwa vizuri bila kupindisha au kuficha ficha wengi hatuko salama.
Dhambi ya zinaa ni dhambi iliyofunga na kuwapoteza watu wengi bila kujali umri,cheo au jinsia. Shetani ameificha dhambi hii kwa kuifanyia "camouflage", kwa namna mbali mbali mfano kutoa tafisiri za uongo na kufanya kampeni za kuhalalisha tendo hili na kuonekana ni kitu cha kawaida watu kufanya bila utaratibu.
Watu wengi wanafikiri kama tendo la Uzinzi au uasherati ni la kawaida na hawajui yaliyo ndani ya hilo tendo sasa Kitabu hiki kitakufungua Ufahamu wa kujua mambo mazito yaliyojificha ndani ya Uzinzi pamoja na uasherati. Hakika kwa Watakaosoma kitabu hiki watafunguliwa fahamu zao.
Watu wengi wamejikuta mateka bila kujua kwasababu ya hili tendo sasa ni wakati wako kupata ufahamu ili uweze kutoka huko kwenye vifungo vizito ambavyo vinauwezo wa kusababisha maisha yako kuwa mazuri au mabaya katika upande wa kiroho na kimwili pia.
Isaya 5:13 "Kwa sababu hiyo watu wangu wamechukuliwa mateka, kwa kukosa kuwa na maarifa; na watu wao wenye cheo wana njaa, na wengi wao waona kiu sana"
Mara tu utakapokipata hiki kitabu kitakufungua akili yako na kitakupa utaratibu wa kutoka katika hiyo hali ya mateka, unaweza ukaona kama masihara lakini sio masihara kuna watu wengi wanateseka kwasababu wamejiingiza katika hivi vifungo vizito na vinawafanya wajione kuwa watu wenye mikosi, laana na hawafanikiwi.
Hosea 4 : 6 "Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako......"
Ndani ya Kitabu hiki nimefafanua kwa kina, kimo, marefu na mapana namna ya hili tendo linavyowatesa wengi na kuzuia mafanikio katika ubaadae wao na kuwafanya kubwa watumwa wa Dhambi. Utakapokubali kusoma kitabu hiki ni hakika utaanza kuona maisha yako yakibadilika.