Huduma ya Ushauri Katika Mtazamo wa Kikristo
Msukumo, mzigo na wito na karama ya kuwasaidia wengine katika kutoka kwenye matatizo yao ni msingi katika huduma ya ushauri, lakini hata hivyo hatuwezi kupuuzia umuhimu wa kufanya ushauri kama taalamu rasmi. Hivyo basi ni muhimu huduma ya ushauri ifanywe kwa kuzingatia vigezo vyote muhimu vya kitaaluma.
Katika kitabu hiki kuna maarifa mengi muhimu ya kuwasaidia watumishi wanaofanya huduma ya ushauri ili waweze kuifanya kwa ufanisi na umahiri. Maeneo muhimu yaliyogusiwa ni kama vile Misingi ya huduma ya ushauri, Aina mbalimbali za ushauri, Njia mbalimbali za kufanya ushauri, Ushauri na Theolojia, Ushauri na Saikolojia, Sifa za mashauri, Maadili ya kufanya huduma ya ushauri, Kanuni na Ujuzi wa ushauri, Hatua za kufanya ushauri na mengine mengi.