Ijue Nguvu ya Kufunga na Kuomba
Wanafunzi wa Yesu waliletewa mgonjwa mwenye kifafa ili wamponye lakini wao walishindwa. Yesu alipopata habari za kushindwa kwao kumponya mgonjwa alisikitika na kisha akamponya mgonjwa.
Wanafunzi hao walipokuwa pamoja na Yesu walimwuliza, "Mbona sisi tulishindwa kumtoa pepo?" Yesu akawaambia kwa namna hii haitoki ila kwa kufunga na kuomba.Rejea Mathayo 17:21
Tunahitaji sana maombi ya kufunga na kuomba katika nyakati hizi za sasa. Kufunga na kuomba hutupa kibali mbele za Mungu na kusikia maombi yetu. Kufunga kiroho ni tofauti na kufanya mazoezi ya kupunguza mwili. Kufunga kiroho huambatana na kuwajali wahitaji, kujinyima chakula, kusoma Neno la Mungu, kufanya ibada na kujinyenyekesha mbele za Mungu. Ukisoma Biblia watumishi wengi walifunga na walipata matokeo makubwa. Ndani ya kitabu hiki utajifunza mambo mengi juu ya kufunga na kuomba.