Jifunze Kiswahili: Kidato cha 1 - 4
Kitabu hiki kinajumuisha mada mbalimbali zenye lengo la kukuza ujuzi wa lugha, fasihi na mawasiliano kwa wasomaji. Katika Kidato cha kwanza mwanafunzi hujifunza msamiati wa kawaida, sharia za lugha, misingi ya fasihi simulizi na fasihi andishi.
Kidato cha pili huendeleza uelewa wa lugha na fasihi hivyo mwanafunzi hujifunza pia uundaji wa maneo katika lugha ya Kiswahili ambao hupelekea kuongezwa kwa misamiati katika lugha.
Kidato cha tatu na nne huleta mada Zaidi za fasihi, uhakiki pamoja na utungaji. Vipengele kama vile riwaya, tamthilia na mashairi hujadiliwa kwa undani Zaidi. Wanafunzi hujifunza jinsi ya kufanya uchambuzi wa kazi za fasihi na kuzitasiri. Kuelewa na kutumia Kiswahili kwa mawasiliano ya kina na kuandika lengo kuu.
Kitabu hiki hujumuisha historia ya lugha, mchango wa fasihi katika jamii na maendeleo ya lugha ya Kiswahili kama lugha ya taifa. Hatua kwa hatua , wanafunzi hupata ujuzi wa kuchanganua, kuelewa, kutoa maoni kuhusu kazi za fasihi, na hii huandaa msingi imara kwa matumizi ya lugha hiyo katika Maisha yao ya kila siku.