Kilimo cha Bustani kwa Wanafunzi kuanzia miaka 8 - 15
Kitabu hiki kinalenga kusaidia wanafunzi kuanzia miaka 8 hadi 15 kuongeza maarifa ya uzalishaji wa mbogamboga katika maeneo wanayoishi kama sehemu ya stadi za maisha.
Pia kitabu kimelenga kusaidia wanafunzi wawe msaada kwa familia zao kipindi cha likizo kwa kuanzisha bustani nyumbani badala ya kutumia muda wao wa mapumziko kucheza na wengine kuangalia vipindi kwenye televisheni visvyo na tija kwa maisha yao ya baadae.
Vilevile, tunao vijana wengi katika jamii wanaoamini kuwa bila ajira rasmi hawawezi kutimiza ndoto zao. Hii inapelekea vijana wengi kushinda mitaani bila shughuli yoyote ya kufanya wakisubiri ajira rasmi. Vijana hawa wakiwa na elimu hii ya bustani tangu wakiwa na umri wa miaka 8, maarifa haya yatakuwa msaada kipindi cha uhitaji wa ajira.
Mwandishi aliamau kuandika kitabu hiki iwe chachu kwa wanafunzi kupata ujuzi na maarifa ya kujishughulisha na kilimo cha bustani ili wawe msaada nyumbani na kwa maisha yao ya badae. Mzazi au Mlezi unashauriwa kununua kitabu hiki kimfae mwanao mapema kwa kuanza kujifunza kilimo cha bustani.